Posts

Showing posts from September, 2023

WAZIRI MAKAMBA AKABIDHIWA RASMI OFISI

Image
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba akikabidhiwa nyaraka mbalimbali na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Stergomena Tax katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. January Makamba (Mb.) amekabidhiwa ofisi rasmi na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb.) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.   Akizungumza wakati  wa  m a kabidhi ano hayo, Mhe. Waziri Makamba amemshukuru Dkt. Tax kwa ushirikiano aliompatia wakati wote tangu yalipofanyika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri mwishoni mwa mwezi Agosti 2023.   “Tangu Mheshimiwa Rais alipofanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri umekuwa ukinipatia ushirikiano wakati wote, nakushukuru sana, pia nakutakia heri katika majukumu yako mapya” amesema Waziri Makamba   Naye Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Tax amesema alipohu...

DKT BITEKO AZINDUA KITUO CHA TAIFA CHA UBUNIFU NA MAFUNZO YA TAAARIFA ZA KIJIOGRAFIA

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko akikata utepe kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 9 Septemba 2023.   Na  Munir Shemweta, WANMM   Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amezindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia na kuitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kujitathmini katika utekelezaji majukumu yake ya msingi badala ya kuwa wizara ya inayoshughulika na utatuzi wa migogoro.   Dkt Biteko amesema hayo tarehe 9 Septemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe.Kassim Majaliwa.   “Kazi kubwa ya Wizara hii ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, sasa tujipime na tujitathmini kama katika sekta yetu ya ardhi kazi hizi tunazifanya kwa ukamilifu wake’’ alisema.   Aidha, ameitaka Wizara ...

TUJENGE NIDHAMU YA WIZARA- WAZIRI SILAA

Image
  TUJENGE NIDHAMU YA WIZARA- WAZIRI SILAA Na  Munir Shemweta, WANMM Waziri wa Ardhi Nyumba na Maeleo ya Makazi Jerry Silaa amewataka watumishi wa Wizara yake kuhakikisha wanawahudumia vizuri wananchi ili wajenge imani na serikali. ‘’Lazima tutengeneze ‘despline’ ya wizara kwa kuwahudumia vizuri wananchi, tukumbuke hapa tunafanya kazi ya watanzania kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan’’ alisema Waziri Silaa. Akizungumza na watumishi wa Wizara ya Ardhi baada ya uzinduzi wa Kituo  cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya Taarifa za Kijiografia, Waziri Silaa amesema,  wakati wa kutekeleza majukumu, watumishi hao wakumbuke kuwa siyo kila mwananchi ana haki lakini wanao wajibu wa kutenda haki wakati wote wa utekelezaji majukumu. ‘’Mna wajibu wa kusimamia haki na kila mtu atolee maamuzi kwa kazi inayowasilishwa kwake na kama mwananchi hapaswi kupewa kiwanja aelezwe bayana kwa maandishi’’ alisema. Kwa mujibu wa Waziri wa Ardhi, wizara yake kwa sasa inakwenda kufanya maboresho ya...

Biteko aipongeza Timu ya Serikali ya Majadiliano kuhusu mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia (GNT)

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na Timu ya Serikali ya Majadiliano kuhusu mradi wa kuchakata na kusindika Gesi Asilia (GNT) ili kufahamu hatua zilizofikiwa kuhusu majadiliano hayo. Dkt. Biteko amekutana na timu hiyo tarehe 9 Septemba, 2023 katika Ofisi za Wizara ya Nishati, Jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ameipongeza timu hiyo kwa kazi kubwa waliyoifanya hadi hatua iliyofikiwa mpaka sasa. Katika kikao hicho Dkt. Biteko ameielekeza GNT kukutana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikiali, inayoshughulika na mikataba ili kuwaeleza kwa kina maendeleo na hatua iliyofikiwa hadi sasa. Dkt. Ameitaka Timu kuwa huru katika kupokea mawazo kila mmoja katika kujenda uelewa wa pamoja wanapotaka  kukubaliana masuala mbalimbali. Ametaka timu hiyo kuongeza kasi ili kukamilisha majadiliano hayo ili mradi huo uanze kutekelezwa kwa kuwa wananchi wanausubiri kwa hamu kubwa kutokana na umuhimu wake kwao na Taifa kwa jumla. Kikao hicho pia kilihudhuri...